POLISI
Tuko Tayai Kumhoji Miguna
Idara ya polisi imemtaka aliyekuwa mshauri wa Waziri Mkuu Miguna Miguna kuandikisha taarifa iwapo idara hiyo itapokezwa barua rasmi na mkurugenzi wa mashtaka ya umma Keriako Tobiko. Akihutubu kwenye kikao na wanahabari, naibu msemaji wa polisi Charles Owino amesema kuwa kila Mkenya anataka haki kutendeka kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu uliopita na kusema kuwa ni sharti Miguna aandikishe taarifa kuhusu madai aliyoyatoa kuwa ana ufahamu kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu uliopita. Ni hivi majuzi tu ndipo Miguna alizindia kitabu kwa jina PEELING BACK THE MASK ambacho kinaendelea kuibua hisia mbalimbali humu nchini.
Posted on July 18, 2012 na Beatrice Maganga
