PODCASTS

Habari

  • Makamishna

    Utafiti wa Gallup

    Utafiti uliofanywa na Kampuni ya Gallup Afrika unaonyesha kuwa asilimia 60.9 ya Wakenya wanaunga mkono uteuzi wa makamishna wa kaunti uliofanywa na Rais Mwai Kibaki na kubatilishwa na mahakama kuu. Kulingana na ripoti hiyo, asilimia 35.8 ya Wakenya wanaopinga uteuzi huo huku asilimia 3.4 wakikosa kutoa mitazamo yao. Utafiti huo uliofanywa kati ya mwezi Juni 12 na 25 pia unaonyesha kuwa asilimia 55.9 ya Wakenya ndio wanaoelewa majukumu wa wakuu wa wilaya, maafisa wa wilaya na machifu. Ripoti hii imetolewa wakati ambapo afisi ya Rais inaelekezewa shutuma kwa madai ya kubeza uamuzi wa mahakama kwamba uteuzi huo ulifanywa kinyume cha sheria.

    0 Responses

    Posted on July 15, 2012 na Victoria Amunga

Comments in chronological order (Total 0 comments)



1100 characters remaining