Moto
Kiwanda Chashika Moto-Dandora
Mali yenye thamani isiyojulikana imeteketea baada ya kiwanda cha kutengenezea magodoro kushika moto katika Mtaa wa Dandora hapa jijini. Inaarifiwa kuwa moto huo ulianzia katika chumba kimoja kabla ya kuenea katika vyumba vingine na kuteketeza magodoro kiwandani humo. Maafisa wa polisi wanasema huenda moto huo ulisababishwa na hitilafu za nguvu za umeme. Hakuna yeyote aliyejeruhiwa katika kisa hicho.
Posted on July 15, 2012 na Zaubeida Koome
