PODCASTS

Habari

  • Ugaidi

    Vilipuzi-Kemikali Zanaswa

    Maafisa wa polisi wanamchunguza mfanyabiashara mmoja aliyepatikana na kilo kadhaa za kemikali inayoweza kutumiwa kutengeneza vilipuzi Mtaani Kariobangi hapa jijini Nairobi. Mfanyabiasha huyo amejitetea kwa kusema amekuwa akiuza kemikali hiyo kwa muda sasa. Licha ya madai hayo, maafisa hao wamechukua kemikali hiyo katika kituo cha polisi cha Buruburu na sampuli nyingine kupelekwa katika maabara ya serikali kwa uchunguzi zaidi. Alhamisi iliyopita maafisa wa polisi walinasa kilo kadhaa za kemikali inayotumiwa kutengeneza mabomu katika mpaka wa Namanga na hadi sasa wanasaka watu wawili waliokuwa na kemikali hiyo.

    0 Responses

    Posted on July 15, 2012 na Zubeida Koome

Comments in chronological order (Total 0 comments)



1100 characters remaining