PODCASTS

Habari

  • Uvamizi

    Polisi Washambuliwa Mandera

    Maafisa wawili wa polisi wamejeruhiwa vibaya baada ya gari lao kumiminiwa risasi na watu waliokuwa wamejihami Mjini Mandera. Gari hilo linalomilikiwa na afisa mkuu wa polisi katika eneo la Mandera Mashariki, lilikuwa likielekea Garissa kutoka Mandera kabla ya kumiminiwa risasi katika eneo la Fino. Dereva wa gari hilo alipigwa risasi mkononi kabla ya gari hilo kupoteza mwelekeo. Maafisa hao wa polisi walikuwa wakielekea Garissa kwenya halfa ya kumkabidhi afisi mkuu wa polisi Mkoani Kaskazini Mashariki, Philip Tuimur anayechukua nafasi hiyo iliyotwaaliwa na Leo Nyongesa. Waliojeruhiwa wanaendelea kupokea matibabu katika Hospitali Kuu Wilayani Mandera.

    0 Responses

    Posted on July 12, 2012 na Mate Tongola

Comments in chronological order (Total 0 comments)



1100 characters remaining