AFYA
UNICEF Kushirikiana na Kenya
Shirika la Umoja wa Mataifa Kuhusu Watoto, UNICEF limeahidi kushirikiana na serikali ya Kenya kwa lengo la kupunguza vifo vya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano. Katika kikao na wakurugenzi wa Shirika la Habari la Standard, mwakilishi wa UNICEF Kanyankore Marcel amesema UNICEF imejitolea kukabili changamoto zinazowakabili akina mama wakati wa kujifungua ili kuhakikisha kuwa malengo ya milenia yanaafikiwa ifikiapo mwaka 2015. Wakati huo Marcel ametoa wito kwa serikali kushirikiana na sekta za nafsi na mashirika ya jamii ili kuhakikisha kuwa ndoa za mapema kwa wasichana zinapunguzwa. Naye Mkurugenzi wa Oparesheni katika Standard Group Savjeet Chana amesema serikali ina jukumu la kuhakikisha kila mtoto anapata mahitaji ya kimsingi. Kulingana na ripoti ya Benki ya Dunia, Kenya ni mojawapo ya mataifa yaliyopiga hatua Barani Afrika katika kupunguza vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano.
Posted on July 12, 2012 na Tabitha Rotich
