PODCASTS

Habari

  • Uhamiaji

    Wakenya Wakamatwa Sudan

    Wakenya sita wanaendelea kuzuiliwa katika kambi moja ya jeshi nchini Sudan Kusini. Wakenya hao ambao wamekuwa kizuizini tangu Ijumaa walitiwa nguvuni baada ya afisa mmoja wa jeshi la Sudan Kusini kudai kwamba walimwibia bunduki na pesa. Habari zasema kuwa Wakenya hao walikuwa safarini kuja nchini na walikuwa katika eneo la Torit walipotiwa nguvuni katika kituo cha ukaguzi cha Kapoeta. Kwa mujibu wa Mkenya mmoja ambaye aliponyoka mnaso huo, Wakenya kumi na raia 15 wa Sudan Kusini walitiwa nguvuni lakini raia wa Sudan waliachiliwa baadaye huku wao wakihangaishwa na hatimaye pesa na simu zao kuchukuliwa kabla ya baadhi yao kuachiliwa huru. Mkuu wa wilaya ya Turkana Kaskazini Patrick Mwirira anadai kutofahamu kisa hicho.

    0 Responses

    Posted on July 12, 2012 na Tabitha Rotich

Comments in chronological order (Total 0 comments)



1100 characters remaining