PODCASTS

Habari

  • Siasa

    Wanjiru Aladwa wapatana

    Siasa za chama cha ODM zimepata mwamko mpya. Hii ni baada ya mirengo ya chama hicho iliyozozana kwa kipindi kirefu katika Kaunti ya Nairobi kuafikiana kufanya kazi kwa pamoja. Akiongea kwenye kikao cha wajumbe wa chama hicho mjini Nairobi, mbunge wa Starehe Bi. Margaret Wanjiru amesema tofauti kati yake na meya George Aladwa sasa hazipo tena na kwamba watashirikiana ili kuyafanikisha malengo ya chama hicho.

    Kwa upande wake Naibu Kiongozi wa ODM ambaye pia mbunge wa Tinderet Henry Kosgey amewahimiza wafuasi wa chama hicho waungane. Kosgey amesisitiza kuwa Kenya inahitaji umoja hivyo basi ni vyema wakenya wa jamii zote waishi kwa utangamano.

    Wakati uo huo naibu waziri mkuu Musalia Mudavadi amesema yuko tayari kushirikiana na vyama vingine wakati wa uchaguzi mkuu ujao licha ya shinikizo kutoka kwa baadhi ya viongozi wa jamii ya Waluhya wanaomtaka asubiri uamuzi wa viongozi wa jamii hiyo kuhusu watakayemuunga mkono kugombea urais.

    0 Responses

    Posted on July 10, 2012 na Ali Haji Kipapuro

Comments in chronological order (Total 0 comments)



1100 characters remaining