PODCASTS

Habari

  • Ugaidi

    Kilo 85 zaidi za poda ya mabomu

    Mahakama imedinda kuwaachilia kwa dhamana raia wawili wa Iran washukiwa wa ugaidi. Hii ni baada ya Kitengo cha Pilisi wa Kukabiliana na Ugaidi kuishawishi mahakama kwamba wawili hao walioingia humu nchini kama watalii ni magaidi hatari. Polisi wamesema wanaamini kuwa wawili hao waliowaelekeza katika sehemu ambako walikuwa wameficha kilo 15 za poda ya kutengeneza mabomu ni hatari kwa sababu inashukuwa walikuwa wameingiza kilo 100 ya poda hiyo nchini.

    Kufikia sasa haijulikani kilo 85 iliyosalia iko wapi. Afisa aliyewakilisha polisi mahakamani Erick Opagal amemwambia hakimu mwandamizi Paul Biwott kwamba kuwaachilia wawili hao kutakuwa sawa na kuwaruhusu kwenda kumaliza kilichowaleta nchini.

    Ufichuzi wa polisi kuwa kilo 100 ya poda hatari ya RDX iliingizwa humu nchini unajiri saa chache tu baada ya serikali ya Marekani kutoa tahadhari nyingine kwa raia wake kutozuru eno la Kaskazini Mashariki ya Kenya.

    0 Responses

    Posted on July 10, 2012 na Bernard Oginga

Comments in chronological order (Total 0 comments)



1100 characters remaining