PODCASTS

Habari

  • Ugaidi

    Marekani Yatoa Tahadhari Tena

    Serikali ya Marekani imetoa tahadhari nyingine inayohusiana na usalama wa Kenya. Nchi hiyo imewaonya raia wake dhidi ya kuzuru maeneo ya Kaskazini Mashariki mwa nchi.

    Serikali hiyo imewatakaza raia wake kuzuru maeneo ya Elwak, Wajir, Garissa, Dadaab, Mandera, na Liboi. Ilani hiyo ya Marekani inajiri siku chache tu baada ya kutoa ilani nyingine kama hiyo ikiwataka raia wake kutozuru mji wa Mombasa na Lamu mkoani Pwani. Ubalozi wa Marekani humu nchini umesema kuwa misururu ya mashambulizi ambayo yameshuhudiwa humu nchini inaashiria utovu wa usalama wa kutosha humu nchini.

    Ni takriban juma mmoja tu tangu watu 17 walipouawa katika mashambulizi dhidi ya makanisa mawili mjini Garissa huku wengine zaidi ya 60 wakijeruhiwa. Inaaminika mauaji hayo yalitekelezwa na wanachama wa kundi gaidi la Al Shabaab.

    0 Responses

    Posted on July 10, 2012 na Beatrice Maganga

Comments in chronological order (Total 0 comments)



1100 characters remaining