ICC
Lubanga Miaka 8 Gerezani
Mahakama ya mataifa jinai ICC imemhukumu miaka 14 gerezani Thomas Lubanga, raia wa Jamuhuri ya Demokrasia ya Kongo anayeshutumiwa kwa kuwatumia watoto kwenye vita vilivyozuka katika taifa hilo. ICC imesema kuwa hukumu hiyo ilianza tarehe 14 mwezi Machi mwana 2006 wakati Lubanga alipojisalimisha mbele yake na hivyo Lubanga amesaza miaka 8 ya kuhudumu gerezani. Lubanga atafungwa Uholanzi.
Lubanga mwenye umri wa miaka 51, alipatikana na hatia mwezi Machi mwaka huu kwa uhalifu wa kivita hususan kwa kuwatumia watoto kama majeshi kati ya mwaka 2001 na 2003. Kamanda huyo wa zamani wa waasi alipatikana na hatia ya kuwahusisha watoto hao wenye umri wa chini ya miaka 15 kwenye vita hivyo vya kaskazini mwa Kongo eneo ambalo lina utajiri mkubwa wa dhahabu na kusababisha vifo vya zaidi ya watu elfu sitini mwaka 1999.
Hii ndiyo kesi ya kwanza ya aliyekuwa mwendesha mashtaka mkuu wa ICC Luis Moreno-Ocampo kukamilika kwa hukumu.
Posted on July 11, 2012 na Mate Tongola
