PODCASTS

Habari

  • Haki

    ICC Yatangaza Tarehe za Kesi

    Mahakama ya mataifa ya Jinai ICC imetangaza tarehe ya kuanza kwa kesi dhidi ya Wakenya wanne wanaokabiliwa na mashtaka kuhusiana na ghasia za baaada ya uchaguzi mkuu uliopita. Kesi dhidi ya mbunge wa Eldoret Kaskazini William Ruto na mwanahabari Joshua Sanga imeratibiwa kuanza tarehe 10 Aprili mwaka ujao huku ile ya Uhuru Kenyatta na Francis Muthaura ikianza tarehe siku moja baada ya hapo yaani tare11 Aprili. Taarifa iliyotolewa na ICC inasema hatua hiyo imechukuliwa ili kutoa muda wa kutosha kwa pande huskika katika kesi hiyo kuandaa ratiba na harakati zitakazofuatwa katika kesi hizo. Kesi hizo zitaanza takriban mwezi mmoja baada ya uchaguzi mkuu ulioratibiwa kufanyika tarehe 4 Machi mwakani.

    Kwa sababu mahakama hiyo huwahitaji kuwepo Hague kesi zao zinapoendelea, huenda harakati za wanasiasa wanaotaka kuwania urais zitatizika katika duru ya pili ya uchaguzi ikiwa wataruhusiwa kugombea katika duru ya kwanza.

    0 Responses

    Posted on July 10, 2012 na Bernard Oginga

Comments in chronological order (Total 0 comments)



1100 characters remaining