PODCASTS

Habari

  • Usalama

    Polisi Wataka Wizara Yao

    Msemaji wa polisi Erick Kiraithe amesema kwamba ipo haja kwa idara ya usalama kutengewa wizara yake mahsusi badala ya kujumuishwa na utawala.

    Akizungumza wakati wa kuzinduliwa kwa ripoti kuhusu hatua zilizopigwa katika mageuzi katika idara ya polisi, Kiraithe amesema iwapo wizara hiyo itabuniwa, polisi watapata fursa ya kukabili mataizo hasa ya kiusalama yanayokabili taifa hili. Kulingana na ripoti ambayo imetolewa na shirika moja linaloshugulikia masuala ya amani kwa jina USALAMA FORUM, kuchelewa katika kuteuliwa kwa Inspekta Mkuu wa Polisi kumesababisha kuchelewa kwa marekebisho katika idara ya polisi. Ripoti hiyo inaonyesa kwamba maafisa wa polisi hawako tayari kukabiliana na visa vya mashambulizi na uhalifu kutokana na ukosefu wa vifaa vya kutosha. Ripoti hiyo inadokeza kwamba juhudi za kutosha hazijaafikiwa kuhakikisa maafisa wa polisi wanapata motisa ya kuimarisha utendakazi wao.

    0 Responses

    Posted on July 9, 2012 na Carren Omae

Comments in chronological order (Total 0 comments)



1100 characters remaining