Mihadarati
NACADA Kutoa Leseni kwa Vituo
Serikali itatoa leseni na kudhibiti vituo vya kuwarekebisha tabia waraibu wa dawa za kulevya kuanzia mwaka huu wa kifedha.
Shirika la kukabiliana na utumizi wa dawa za kulevya NACADA vilevile limesema kwamba mikakati inapangwa kutoa vibali kwa wataalamu wanaowashughulikia watumizi wa dawa za kulevya. Mshirikishi wa NACADA William Okedi amesema hatua hiyo ni njia mojawapo ya kuhakikisha unyoofu katika huduma zinazotolewa.
Okedi alikuwa akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kituo cha kurekebisha tabia kwa watumizi wa dawa za kulevya katika hospitali ya Rufaa ya Moi mjini Eldoret.
Posted on July 9, 2012 na Velmar Mrenje
