Katiba
Wamalwa: Uamuzi wa mahakama ni funzo
Waziri wa Haki na masuala ya Katiba Eugene Wamalwa ameutaja uamuzi wa mahakama kubatilisha uteuzi wa makamishna 47 wa kaunti kuwa funzo kwa Wakenya kwamba mahitaji ya katika lazima yatimizwe.
Waziri huyo amewaonya Wakenya kuwa iwapo hawatatimiza kanuni ya jinsia kama inavyohitajika na katiba katika uchaguzi mkuu ujoa watalazimika kufanya hivyo kwa gharama zaidi. Akizungumza alipohudhuria mazishi ya Sarah Makokha Barasa mamake Naibu Jaji Mkuu aliyesimmaishwa kazi Nancy Barasa kijijini Kimabole wilayani Mount Elgon, Wamalwa amesema uhuru wa mahakama umeanza kudhihirira.
Licha ya uamuzi huo wa mahakama, Katibu katika wizara ya usalama wa Taifa Mutea Iringo amewaagiza makamishna hao kuendelea na kazi akisema Mwanasheria Mkuu Prof. Githu Muigai atakata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa Mahakama Kuu siku ya Jumatatu.
Posted on June 30, 2012 na Robert Wanyonyi
