Mahakama
Iringo; Makimshna wa kaunti waendelee
Katibu katika wizara ya Usalama wa Taifa Mutea Iringo amefichua kuwa Mwanasheri Mmkuu Prof. Githu Muigai atakataa rufaa siku ya Jumatatu kupinga uamuzi wa mahakama kutupilia mbali uteuzi wa makamishna 47 wa Kaunti uliofanywa na rais Mwai Kibaki.
Akiwahutubia makamisha hao katika warsha ya kuanza kazi iliyokamilika katika Chuo cha Mafunzo ya Utawala, KIA siku ya Jumamosi Iringo amewahikishia makamisha hao kwamba wataendelea kuhudumu na kuwaagiza warejee katika vituo vyao na kuendelea kufanya kazi. Vile vile ametilia shaka uamuzi wa mahakama kutupilia mbali uteuzi huo akisema wizara nyingine zimewateua wasimamizi wa Kaunti ilhali utewuzi huo haujapingwa.
Siku ya Ijumaa Jaji wa Mahakama Kuu Mumbi Ngugi alitoa uamuzi kuwa rais alikiuka katiba alipofanya uteuzi huo kwa kupuuza hitaji la jinsia. Kati ya makamisha hao 47 ni kumi tu ndio wanawake. Jaji Ngugi pia alisema rais alikuka makataba wa ugavi wa mamlaka kwa kufanya uteuzi huo bila kushauriana na Waziri Mkuu Raila Odinga.
Posted on June 30, 2012 na Bernard Oginga
