Riadha
Rais Akabidhi Bendera
Rais Mwai Kibaki amewakabidhi bendera wanariadha watakachowakilisha Kenya katika mashindano ya Olimpiki nchini Toronto na Landon mwezi ujao. Kwenye hotuba yake wakati wa hafla hiyo Rais Kibaki ametoa hakikisho kwamba serikali itaendelea kutoa ufadhili kwa vikosi vya riadha na michezo mbalimbali. Amesema tayari mipango hiyo imeanza katika sehemu tofauti nchini kama vile kuzindua kituo cha kutoa mafunzo ya mataifa katika michezo mbalimbali. Rais pia amewapongeza wanariadha hao kwa juhudi zao za kuimarisha taifa hili katika michezo, huku akiwapa changamoto kuhakikisha kuwa wanadumisha nafasi ya Kenya kwenye Olimipiki katika ngazi ya mataifa. Kwa upande wake Waziri wa Michezo Pual Otuoma amesema kikosi hicho kimeteuliwa kwa njia ya uwazi. Aidha amesema wanariadha hao wamepata mafunzo ya kutosha ili kuwaandaa vilivyo. Otuoma amesema wizara yake ameshirikiana na wizara ya elimu kuona kwamba wale ambao wana uwezo wanapata fursa ya kushirikishwa katika mashindano hayo.
Posted on June 27, 2012 na Carren Omae
