Darubini 1.
Serikali, Mzaha Kuhusu Ugaidi
Siku mbili zilizopita, serikali ya Marekani iliwatahadharisha raia wake kuhusu uwezekano wa kutokea kwa shambulizi la ugaidi Mjini Mombasa. Siku moja baadaye, maafisa wa serikali ya Kenya walijitokeza kwa ghadhabu kukana taarifa hizo, mbali na kudai kwamba ililenga kudidimiza sekta ya utalii nchini. Saa chache tu baada ya kukana tahadhari za Marekani, mlipuko ukatokea katika baa moja mjini Mombasa. Je, ni kwa nini serikali hukosa busara ya kuchunguza madai yanayotolewa badala ya kuwa mbioni kuyakanusha? Tunalipa uchambuzi pevu suala hili kwenye darubini yetu leo. Geoffrey Mung’ou anatanguliza sehemu ya kwanza ya darubini hiyo.
Posted on June 25, 2012 na Geoffrey Mung'ou
