PODCASTS

Habari

  • Ubakaji

    Migori-Kijana Mbakaji

    Kijana mwenye umri wa miaka 13 anadaiwa kuwabaka watoto 7 wenye umri wa kati ya miaka miwili na 14 katika kijiji cha Wasweta, Kaunti ya Migori. Inadaiwa kuwa mtoto huyo amekuwa akiwabaka watoto hao kwa muda sasa, na katika kisa cha hivi punde amepatikana akimbaka mtoto mwenye umri wa miaka miwili unusu. Mshukiwa wa vitendo hivyo ambaye jina lake tumelibana alithibitisha kuhusika na vitendo hivyo mbele ya afisa wa watoto katika Kaunti ya Migori, Peter Ogindo na kusema kwamba amekuwa akiiga vitendo vya watoto wengine ambao pia wamekuwa wakishiriki tabia hiyo. Afisa huyo wa watoto amesema mtoto huyo anahitaji ushauri nasaha kwa lengo la kukomesha tabia hiyo mbali na kuwazuia watoto hao dhidi ya kuambukizwa maradhi ya zinaa. Ogindo aidha ametoa wito kwa wazazi kumakinika katika ulezi wa wanao ili wajiepushe na tabia potovu.

    0 Responses

    Posted on June 19, 2012 na Beatrice Maganga

Comments in chronological order (Total 0 comments)



1100 characters remaining