Uchunguzi wa Ajali
Orodha ya Wanajopo
Kwa mara nyingine serikali imewahakikishia Wakenya kwamba uchunguzi wa kina utafanywa kuhusu chanzo cha ajali ya ndege iliyosababisha vifo vya mawaziri Prof. George Saitoti na Orwa Ojode pamoja na Wakenya wengine wanne wiki moja iliyopita. Waziri Mkuu Raila Odinga Jumatatu alasir, alitangaza rasmi jopo la watu 13 litakaloongozwa na jaji wa Mahakama ya Rufaa Kalpana Rawal kufanya uchunguzi wa kina kuhusu ajali hiyo. Baadhi ya masuala yatakayochunguzwa ni pamoja na chanzo cha ajali hiyo, ununuzi wa helikopta iliyohusika katika ajali yenyewe, jinsi ilivyotunzwa na kurekebishwa. Aidha Waziri Mkuu amesema serikali itahakikisha kuwa ripoti ya uchunguzi huo itawekwa wazi ili hatua zinazofaa zichukuliwe kuambatana na mapendekezo ya ripoti hiyo. Waziri wa uchukuzi Amos Kimunya ndiye atakayekuwa msemaji wa serikali kuhusu suala hilo.
Posted on June 19, 2012 na Ali Haji Kipapuro
