Mahakamani
Adai Mutula ni baba ya mwanawe
Mahakama kuu imeagiza kuchukuliwa kwa chembechembe za DNA kutoka kwa mwili wa marehemu seneta wa Makueni Mutula Kilonzo kufuatia agizo la mwanamke kwa jina Eunice Nthenya anayedai kuwa marehemu ni baba mzazi wa mwanawe wa umri wa miaka 7. Jaji Luka Kimaru amesema kuwa chembechembe hizo zitatumika kubaini baba mzazi wa mtoto huyo kwenye kesi iliyowasilishwa mahakamani kupitia chama cha mawakili wa kike FIDA. Nthenya anasema kuwa ni yeye ni mwanawe mmoja wa wafanyikazi wa mwendazake na kwamba alijifungua kijana huyo tarehe 6 mwezi Mei mwaka 2006.
Posted on May 8, 2013 na Mate Tongola
