Wagonjwa
Warejea Hospitalini - Mathari
Wagonjwa watano zaidi waliotoroka kutoka hospitali ya wagonjwa wa akili ya Mathari hapa Nairobi wamerejeshwa hospitalini humo na jamaa zao. Kufikia sasa, idadi ya wagonjwa waliorejea ni 14 kati ya 40 waliotoroka hospitalini humo mapema wiki hii. Wasimamizi wa hospitali hiyo wametoa wito kwa umma wakiwemo wazazi wa wagonjwa 26 ambao kufikia sasa hawajulikani waliko, kuwarejesha hospitlaini ili waweze kuendelea kupokea matibabu.
OCPD wa Starehe Samuel Anampiu ameiambia Radio Maisha kwamba 40 hao walikuwa miongoni mwa 75 waliotoroka kutoka chumba walimokuwa wamefungiwa. Hata hivyo, 35 kati yao walikamatwa baada ya jaribio lao la kutoroka kutofua dafu. Aidha, tisa kati ya waliotoroka walirejeshwa hospitalini humo na jamaa zao mapema jumatatu, huku 7 wakijirejesha wenyewe.
Posted on May 15, 2013 na Mate Tongola
