Mazingira
Uhai wa Ziwa Victoria
Wakazi wa kaunti ya Kisumu wametakiwa kuwashinikiza viongozi wapya waliochaguliwa eneo hilo kushughulikia kwa haraka kusafishwa kwa ziwa Victoria ambalo ni kitega uchumi kwa asili mia kubwa ya wakazi wa eneo hilo. Akitoa wito huu, Jeppe Kolding ambaye ni mhadhiri katika chuo kikuu cha Bergen nchini Norway, amesema kuwa kwa ushirikiano na wenyeji, serikali ina uwezo wa kulisafisha ziwa hilo na hivyo kukabiliana na umasikini ambao unawaadama wenyeji. Mhadhiri huyo ambaye amefanya utafiti kuhusu ziwa Victori kuanzia mwaka 2005, anasema sharti baraza la jiji la Kisumu lishughulikie kwa haraka suala la maji taka ambayo huelekezwa katika ziwa hilo na hivyo kuhatarisha viumbe vya majini wakiwemo samaki. Katika mahojiano ya kipekee na Radio Maisha mjini Kisumu baada ya kongamano la siku mbili lililowaleta pamoja wataalam wa masuala ya uvuvi chini ya mwamvuli wa Kituo cha Kimataifa kinachoshughulikia masuala ya mazingira, ELCI.
Posted on April 19, 2013 na Mate Tongola
