PODCASTS

Habari

  • Usalama

    Visa vya Uhalifu kukomshwa - Uhuru

    Rais Uhuru Kenyatta amewataka makamanda wa polisi kuwachukulia hatua za sheria wale wote watakaohusishwa na vitendo vya utovu wa usalama nchini. Katika mkutano ulioandaliwa katika ikulu ya Rais hapa Nairobi, Uhuru amesisitiza kwamba serikali yake yaitoruhusu utepetevu katika idara ya polisi. Ametoa agizo hilo wkaati kumekuwa na tetesi kwamba baadhi ya wanasiasa wanahusika pakubwa kwenye mashambulizi na mauaji yaliyoshuhudiwa katika kaunti za Busia na Bungoma wiki iliyopita. Duru kutoka mkutano huo wa alhamisi zimearifu kwamba wakuu hao wa polisi walimwarifu rais kuwa wanakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo ukosefu wa vifaa vya kazi, kutokuwepo kwa motishia miongoni mwa polisi na kadhalika. Vile vile, mafisa hao wamemtaka rais Uhuru kusitisha mabadiliko yanayofanyiwa idara hiyo ikiwemo kuteuliwa kwa makamanda wa kaunti. Hata hivyo, Uhuru amewahakikishia wakuu hao kwamba atashirikiana nao kikamilifu ikiwemo kushughulikia kwa haraka chamgamoto zinazowakabili.

    0 Responses

    Posted on May 17, 2013 na Mate Tongola

  • Usalama

    Ruto ahimiza vikosi vya AMISOM viongezwe Somalia

    Naibu Rais William Ruto ametoa wito kwa Umoja wa Afrika AU uongeze vikosi vyake vinavyolinda usalama nchini Somalia, AMISOM. Ruto amesema ukosefu wa usalama nchini humo umeathiri pakubwa ustawi wa mataifa mengine ya kanda ya Afrika Mashariki. Ameyasema hayo alipokutana na marais wa Congo Brazzaville Dennis Sassou Nguesso na mwenzake wa Gabon Ali Bongo katika mataifa yao.

    Kwenye mazungumzo yao marais hao wamesema kuongezwa kwa vikosi vya AMISOM nchini Somalia kutaimarisha usalama nchini humo. Haya yanajiri wakati ambapo taifa la Kenya limekabiliwa na changamoto nyingi za kiusalama yakiwemo mashambulizi ya kigaidi.

    0 Responses

    Posted on May 17, 2013 na Ali Haji Kipapuro

  • Serikali

    Mawaziri wa Jubilee waanza kazi

    Waziri wa Ugatuzi na Mipango Anne Waiguru ameanza rasmi kutekeleza majukumu yake, siku moja baada ya kuapishwa. Kwenye hotuba fupi wakati akiingia afisini katika jumba la Treasury mjini Nairobi, Bi Waiguru ametoa shukrani kufuatia uteuzi wake na kuahidi kutekeleza majukumu yake kikamilifu ili kufanikisha malengo ya serikali ya Jubilee. Waziri huyo amekaribishwa afisini na katibu katika wizara ya mipango Dkt. Edward Sambili. Bi Waiguru amekariri umuhimu wa kuifanyia mageuzi wizara hiyo ili kuhakikisha inatoa huduma bora kwa Wakenya. Kabla ya kuteuliwa kwake katika wizara hiyo Bi Ann Waiguru alihudumu katika wizara ya fedha akiwa mkuu wa kitengo cha Usimamizi. Alikuwa wa kwanza kuhojiwa na kamati ya bunge iliyowachuja mawaziri wateule. Bi Waiguru ana shahada ya uzamifu katika masuala ya uchumi (Economic Policy).

    0 Responses

    Posted on May 16, 2013 na A Haji Kipapuro

  • Uteuzi

    Ban Ki-Moon amteuwa Dr Kituyi

    Sasa ni rasmi kwamba aliyekuwa waziri nchini Kenya Dakt Mukhisa Kituyi atakuwa kiongozo wa shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara UNCTAD. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemteua rasmi Dkt. Kituyi kuwa Katibu Mkuu wa Shirika hilo la Biashara na Maendeleo ulimwenguni. Dkt. Kituyi atahudumu katika wadhfa huo kwa kipindi cha miaka minne kuanzia Septemba 1, mwaka huu. Dkt. Mukhisa Kituyi aliwahi kuwa mbunge humu nchini na pia alihudumu kama waziri wa Biashara na Viwanda. Uteuzi wake utajadiliwa na Baraza la Umoja wa Mataifa na iwapo utaidhinishwa, atachukua nafasi inayoshikiliwa na Supachi Panitchpakdi kutoka nchini Thailand aliyetwaa wadhfa huo mnamo Septemba, 1 mwaka 2005 na kisha akateuliwa tena mwaka 2009. Kipindi chake cha kuhudumu kinatamatika tarehe 31 mwezi Agosti mwaka huu.

    0 Responses

    Posted on May 16, 2013 na Haji Kipapuro

  • Usalama

    Uhuru na wakuu wa Usalama

    Rais Uhuru Kenyatta anakutana na wa wakuu wote wa polisi nchini, kujadili masuala ya usalama wa taifa ikiwemo mbinu za kuimarisha usalama. Mkutano huo katika ikulu ya rais unahudhuriwa na wakuu wa polisi katika maeneo manane ya nchi (PPO) na wenzao wa idara za upelelezi (PCIO). Mkutano huu unajiri wakati usalama umeripotiwa kuzurota katika pembe tofauti nchini hususan Kaskazini Mashariki na magharibi mwa Kenya. Rais anaandaa mkutano huo siku mbili tu baada ya kutoa agizo la kutengwa kwa kima cha shilingi bilioni 4 kila mwaka, fedha zitakazotumika kununua silaha na vifaa vinginevyo katika idara ya usalama.

    0 Responses

    Posted on May 16, 2013 na Mate Tongola

  • Uslaama

    6 watoroka seli za polisi, Tana River

    Polisi wameimarisha msako dhidi ya washukiwa 6 sugu wa uhalifu waliotoroka kutoka seli ya kituo cha polisi cha Gamba, kaunti ya Tana River usiku wa kuamkia alhamisi. naibu kamishna wa kaunti hiyo Mike Kimoko amethibitisha kisa hicho na kuelezea imani yake kuwa waliotoroka watatiwa nguvuni hivi karibuni. Haya yanajiri wakati kuna tetesi kuwa miongoni mwa waliotoroka ni washukiwa wanne wa mauaji ya watu 38 wakiwemo mafisa 9 wa polisi eneo la Kilelengwani, kaunti hiyo ya Tana River mapema mwezi uliopita. Kis ahiki kinajiri siku mbili tu baada ya wagonjwa 40 wa akili kutoroka kutoka hospitali ya Mathari hapa Nairobi. Hata hivyo, baadhi ya waliotoroka tayari wamerejeshwa hospitalini humo na wanaendelea kupokea matibabu.

    0 Responses

    Posted on May 16, 2013 na Mate Tongola

  • Bungeni

    Mzozo wa PAC na PIC wasuluhishwa

    Mzozo uliokumba kubuniwa kwa kamati mbili muhimu za bunge hatimae umesuluhishwa. Wabunge kutoka muungano wa CORD wametangaza kusitisha matakwa yao kuhusu wanachama wa kamati za uekezaji PIC na uhasibu PAC. Sasa Muungano wa CORD umekabidhiwa nafasi 13 katika kamati hizo mbili huku muungano wa Jubilee ukiwa na nafasi 14. Awali, wabunge wa CORD walitangaza kujiondoa kutoka kamati zote za bunge wakishikilia msimamo kuwa lazima Kamati hizo mbili muhimu ziwe na wabunge wengi kutoka upinzani ili kupiga darubini mienendo ya serikali.

    0 Responses

    Posted on May 16, 2013 na Mate Tongola

  • ICC

    Joshua Sang Kuhudhuria vikao ICC

    Mwanahabari Joshua Arap Sang amesema yuko tayari kuhudhuria vikao vya kesi dhidi yake katika mahakama ya Mataifa kuhusu jinai ICC kinyume. Wakili wa Sang, Katwa Kigen ameyaambia mahakama hayo kwamba mteja wake yuko tayari kuhudhuria vikao hivyo siku baada ya nyingine hadi pale uamuzi wa kesi dhidi yake utakapotolewa. Aidha, majaji wa mahakama hayo wanatarajiwa kutoa uamuzi wa iwapo watawaruhusu rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto kuhudhuria vikao hivyo kwa kupitia video wakiwa humu nchini. Wakili wa Ruto alikuwa na wakati mgumu kukabili masuali kutoka kwa majaji wa ICC kuhusu ombi la mteja wake la kutohudhuria vikao vya Hague, akiwamo jaji Jaji Chile Eboe Sujji. Haya yanajiri wakati mwendesha mashtaka wa mahakama hayo Fatuo Bensouda akiwa amewaandaa mashahidi 77 kwenye kesi dhidi ya viongozi hao wawili .

    0 Responses

    Posted on May 16, 2013 na Alfrique Otieno

  • ICC

    Kenya Kushirikiana na ICC Kikamilifu

    Naibu rais William Ruto ameahidi kushirikiana kikamilifu na mahakama ya mataifa kuhusu jinai ICC. Akizungumza jana katika mahakama hayo, Ruto amesisitiza kuwa atathibitisha kuwa hana hatia kutokana na imani yake katika sheria. Ruto ambaye amekuwa kiongozi wa kwanza wa ngazi za juu serikalini kuhutubia mahakama ya ICC, hata hivyo ametoa wito kwa majaji wa ICC mahakama kuzingatia kwa usawa majukumu yake kama naibu rais na pia kama mshukiwa wa mahakama hayo. Akijieleza kwenye kikao kilichofanyika jumanne jioni katika mahakama hayo yenye makao yake Uholanzi, Ruto amesisitiza kwamba serikali mpya ya Kenya imejitolea kushirikiana na ICC na kuongozea kwamba pamoja na rais, wana imani katika sheria, haki na ukweli. Wakili wa Ruto Karim Khan aliwasilisha hoja zake kutaka tarehe ya kuanza kusikilizwa kwa kesi dhidi ya Ruto iahirishwe hadi mwezi Novemba. Vile vile ,wakili wa mwanahabari Joshua Sang -Katwa Kigen ameitaka ICC kuwapa nafasi ya kutosha kujiandaa kikamilifu.

    0 Responses

    Posted on May 15, 2013 na Alfrique Otieno