×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Moha Jicho Pevu: Vita dhidi ya Governor Joho ni makabiliano ya kisiasa

News
 President Uhuru Kenyatta has a word with Governor Hassan Joho during the launch of the Port Reitz/ Moi International Airport Access road in Mombasa County

Yeyote azuiae riziki ya mwenzake kwa misingi ya kibepari, kabila ni hayawani mkubwa asiyestahili heshima.

Majuzi nikitazama runinga niliona vilio vya zaidi ya wafanyakazi mia tano wakililia haki zao za ajira baada ya kampuni mbili zinazohusishwa na familia ya Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho kufungwa ghafla na mtu fulani. Sitaki kusema serikali ilihussika, lakini ni wazi kuwa aliyetoa maamuzi hayo alikuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa — kumbuka mtu huyu alikataa kufuata maamuzi ya mahakama iliyoamuru kampuni hizo mbili za Autoports Freight handlers limited na Portside kufunguliwa.

Je, ni nani huyu mkubwa mwenye mbwa asiyetaka kuheshimu mahakama za Kenya? Disemba mwaka uliopita Rais Kenyatta alipiga kambi Mombasa bila hata kumjulisha Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho. Rais aliendeleza shughuli zake kwa makini. Baadaye waliishia kutumia jukwaa moja na Gavana wa Mombasa kule Shika Adabu, Likoni. Joho bila kusita alimwambia si vyema yeye kama kiongozi kutomuhusisha na mambo ya pwani ilhali yeye ndiye gavana wa eneo hilo.

Hapa ndipo matusi yalianza jukwaani huku Ali Hassan Joho akitumia hekima kumjibu seneta wa Nairobi Gideon Mbuvi Sonko aliyeonekana kutokwa na matamshi ya ki-ajabu mbele ya watoto, kina mama na wazee. Rais kwenye kanda za video alionekana kucheka na kufurahia yaliyokuwa yakijiri. Hayo yalizikwa katika kaburi la sahau. Iliyofuatia, wiki kadhaa baadaye, ni kule kufutiliwa mbali kwa leseni ya kampuni zinazo husishwa na familia ya Joho. Baadaye halmashauri ya utozaji ushuru KRA ilitoa taarifa na kusema kampuni hizo zilikwepa ushuru.

Iwapo wao ndio wanaotoza ushuru na kubaini yaliyondani ya kontena, kwa nini kumsulubisha mtu asiye na mamlaka hiyo? Hii sio mara ya kwanza kwa bidhaa kunaswa. Sukari zilizodaiwa kunaswa zilipatikana katika vituo vingine nane ikiwemo bandari ya pwani. Ni kwa nini walichagua familia ya Joho? Je, hii ni hila dhidi ya Joho ambaye amekuwa akimuunga mkono kiongozi wa upinzani Raila Odinga? Anachofanyiwa Joho ni sawia na alichofanyiwa Mzee Keneth Matiba miaka ya nyuma.

Hii ni vita vya ubabe wa chama na mojawapo ya njia ya kujaribu kumkata maguu ndugu Joho. Hii ni sawia na kuwalazimisha wapwani kupigia kura Jubilee la sivyo wafungiwe biashara na hata usafiri.

Mimi nahofia kesho. Naogopa keani kesho mtawalenga wengi wengi katika misingi finyu na zisizo na mpangilio wowote.

Mohammed Ali ni Mhariri Mkuu wa Kitengo cha Upekuzi KTN. Kuwasiliana naye: [email protected], FB: Official Jicho Pevu with Mohammed Ali, Twitter: @mohajichopevu

Related Topics


.

Popular this week

.

Latest Articles