Jaguar matatani

Na Mate Tongola

NAIROBI, KENYA, Idara ya Upelelezi, CID inaendeleza uchunguzi wa kubaini iwapo baadhi ya maafisa wa usalama wanaficha ukweli kuhusu ajali iliyomhusisha mwimbaji Charles Kanyi, maarufu Jaguar ambapo watu wawili waliaga dunia.

uchunguzi huo unafuatia agizo la Mkuu wa Mashtaka ya Umma, Keriako Tobiko ambaye amemtaka Murugenzi wa Idara ya Upelelezi, Ndegwa Muhoro kuchunguza kisa hicho cha Jumanne wiki hii, ambapo gari la Jaguar aina ya Range Rover Sport liliwagonga wanaume wawili waliokuwa wakisafiria pikipiki, kwenye Barabara Kuu ya Makutano - Sagana.

Walioshuhudia wanasema mwanamke mmoja ndiye aliyekuwa akiliendesha gari hilo kutoka Sagana kuelekea Makutano. Hata hiyo Jaguar amesisitiza kwamba yeye ndiye aliyekuwa akiliendesha gari hilo.

Related Topics

Jaguar CID