Maafisa zaidi ya 100 wa trafiki waachishwa kazi

Na Suleiman Yeri

Tume ya Huduma za Polisi, NPSC imewaachisha kazi maafisa wa trafiki 127 miongoni mwa maafisa takribani 900 waliochujwa. Maafisa hao walikosa kuafikia vigezo vilivyowekwa.

Hayo yakijiri, aliyekuwa Msemaji wa Polisi Masoud Mwinyi aliyeachishwa kazi mwaka jana, amerejeshwa kuhudumu katika idara ya polisi.

Mwinyi ni mmoja wa maafisa sita miongoni ishirini waliorejeshwa kazini baada ya kutuma maombi ya kupinga hatua ya NPSC kuwafuta na kutaka kufanyiwa uchunguzi upya.

Maafisa wengine kumi na wawili hawajaruhusiwa kuendelea kuhudumu huku mmoja akiwa na kesi mahakamani na mwingine kutuma ombi la kustaafu ambalo tume hiyo imeridhia.

Related Topics

NPSC Masoud Mwinyi