Waziri wa fedha Njeru Githae na washika dau wa muungano wa walimu humu nchini KNUT, wametia sahihi mkataba jumapili tarehe 23 mwezi 2012 unaoahidi usawazanishaji wa marupurupu ya walimu tangu mwezi julai mwaka 2012. Huku wanafunzi wakikosa masomo yao kwa wiki tatu, uzito wa mkataba huo utahisiwa pale wanachama wa kongamano la kitaifa watakapoukubali mkataba huo na hatimaye kuusitisha mgomo huo