Jaji joyce Khaminwa na Jean Gacheche hawatohudumu tena kama majaji katika mahakama,hii ni baada ya bodi ya uchujaji majaji kusema kwamba hawastahili kuhudumu huku kila mmoja wao akipewa sababu zake , naye jaji mohamed ibrahim wa mahakama ya juu, na Roselyn Nambuye wa mahakama ya rufaa watachunguzwa upya . Uamuzi huo umetolewa na bodi ya uchunguzi wa majaji baada ya rufaa zao kwa bodi hiyo kukubaliwa.