Wanachama wa chama cha wenye vyombo vya habari nchini wamemuandalia naibu mwenyekiti wa shirika la the Standard Group na afisaa mkuu anayeondoka paul Melly dhifa ya kipekee ya kwaheri katika hoteli ya kentmare mjini limuru . Wasimamizi wa mashirika mbalimbali ya habari nchini walimsifu melly kwa utendaji kazi wake . Wakatihuohuo wasimamizi hao walitaja umuhimu wa vyambo vya habari hasa wakati huu ambapo kenya inajiandaa kwa uchaguzi mkuu . Afisaa mkuu wa shirika la standard group aliyechukua nafasi ya melly sam sholei amesema kuwa atajitolea vilivyo kuhakikisha kuwa shirika hili litaendelea kufanya vyema hasa katika uana habari .