Aliyekuwa wakati mmoja kamanda wa kikosi cha polisi kinachomsindikiza rais, Elijah Sumbeiyo, ameaga dunia. Marehemu Sumbeiywo alifariki mishale ya saa kumi asubuhi. Alikuwa akiuguza ugonjwa wa saratani ya kongosho ama ‘pancreas cancer’ kwa lugha ya kiingereza. Wakati huo huo, aliyekuwa wakati mmoja waziri na mbunge wa Githunguri Arthur Magugu pia ameaga dunia mchana wa leo mwendo wa saa tano asubuhi