Kampeni za uchaguzi zinapoingia kileleni kawaida ya wanasiasa huwa ni kuwaendea wapiga kura na ahadi tele, zikiwemo ahadi za kuinua hadhi ya maeneo fulani, kutoa nafasi za ajira serikalini na kuimarisha maendeleo na kadhalika. Lakini historia imeonyesha kwamba wadhifa wa makamu wa rais ndio umekuwa ukitumiwa sana kuwarai wapiga kura. Lakini sasa wanasiasa wanaonekana kusakamwa na masharti yaliyonakiliwa chini ya katiba mpya na hivyo kuwaacha baadhi ya wakitapatapa. Je ni nini watakachotumia kama chambo cha kuvutia wapiga kura msimu huu? Ndio hoja uinayotupambia makala yetu maalum ya kila juma ya kinyanganyiro.