Mtazamaji, ushampeleleza mwanao kuwa na upungufu wowote haswa wa kimasomo. Hii humsababisha asifanye vizuri kwenye mitihani au hata kutoelewa anayofunzwa shuleni? Basi pengine haujakuwa makini kuufahamu upungufu huo unaohitaji masomo maalum. Katika makala yetu maalum tunaangazia jinsi ya kuwagundua wanafunzi kama hawa na mambo ya kuzingatia ili kuimarisha ufahamu wao wa masomo.