Ugonjwa wa saratani umeongezeka kwa kiwango kikubwa miaka ya hivi karibuni, ni kana kwamba kuna mkurupuko wa saratani, hali ya matibabu ya ugonjwa huo ni ghali mno na ni wale wenye mali wanaoweza kugharamia hayo na wale wanaokosa matibabu ni wale wenye kuishi na umaskini vitongojini na hata mashambani.
Shirika moja linalohamasisha umma kuhusu ugonjwa wa saratani limezindua kampeini mpya kwa jina “99 days of cancer” ambayo itasaidia kuhamasisha umma na kushinikiza serikali kuvipa nguvu vituo vya afya kuwatibu wagonjwa wa saratani kwa bei nafuu . Taarifa ifuatayo inaeleza taswira kupitia mama mmoja anayeishi na saratani .