Maafisa wa polisi mjini Naivasha, wanawazuilia wazazi wawili kwa kusababisha kifo cha mtoto wao. Yadaiwa kuwa wazazi hao walikataa katakata kumpeleka mtoto wao hospitalini pamoja na wenzake sita walipopatikana na ugonjwa wa ukambi wakisema dini yao haiwaruhusu kupewa matibabu.