Jopo-kazi linalopigia msasa kesi za machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu wa 2007 limedokeza kuwa litapendekeza mahakama maalum ibuniwe kwa minajili ya kuwafungulia mashtaka washukiwa wa ubakaji na mauaji. Mwenyekiti wa jopo-kazi hilo, wakili Dorcas Oduor amesema sheria maalum pia zitatumiwa kwenye mahakama hiyo, ikiwemo ile ya makosa ya jinai za kimataifa ili kuhakikisha waathiriwa wa ubakaji na mauaji wanatendewa haki. Kwa taarifa kamili huyu hapa Patrick Amimo.