Wachimba migodi 30 wameuawa nchini Afrika Kusini kwa kupigwa risasi na maafisa wa polisi huku kadhaa wakijeruhiwa katika juhudi za kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakilalamikia mishahara duni. Wachimba migodi hao waliokuwa wakiandamana nje ya mgodi wa Lonmin Platinum wa Marikana, waliuwawa kinyama huku polisi wakidai kuwa ilikuwa ni juhudi za kuwatawanya. Na kama anavyotuarifu mwanahabari wetu Mohamed Mahmoud, ni mauaji yaliyoimarisha uhasama kati ya maafisa wa polisi na wachimba migodi.