Kampuni ya kutengeneza pesa nchini de la rue hii leo imejitetea kuwa hakuna pesa zozote zilizopotea kutokana na kufutiliwa mbali kwa kandarasi waliyokuwa wamekabidhiwa ya kuchapisha noti mpya na za kisasa, baada ya aliyekuwa waziri wa fedha amos kimunya kufutilia mbali kandarasi hiyo. Kampuni hiyo pia imeilaumu kamati ya bunge inayohusika na fedha za umma kwa kutotilia maanani baadhi ya ripoti waliyowapa wakati walipohudhuria baadhi ya vikao vyake hivyo basi kupoteza ukweli wa mambo. Hata hivyo, kufikia sasa ukweli kamili haujabainika kama kweli serikali ilipoteza fedha hizo kwa kutupilia mbali kandarasi hiyo, kwa sasa kampuni hiyo inasisitiza kuwa haina shinikisho zozote kutia sahihi mkataba mwingine na serekali ya kenya ya kutengeneza noti hizo za kisasa na badala yake imekariri kuwa itaendelea kuchapisha noti za zamani.