Tahadhari iko juu mjini Mombasa baada ya mtu mmoja kufikishwa na kulazwa katika hospitali ya Aga Khan akionyesha dalili za ugonjwa wa ebola. Mtu huyo ambaye ni dereva wa magari ya mizigo anakiri kuwa nchini Uganda wiki imepita akifika hospitalini kutibiwa alichodhania ni homa kali. Licha ya kuwa uchunguzi umeanzishwa katika maabara ya kemri kudhibitisha anachougua, mgonjwa huyo pamoja na wengine watatu waliotangamana naye wametengwa katika hospitali hiyo huku taharuki ikitanda. Esther Kahumbi anaripoti kutoka Mombasa.