Huku mahakama ikiwa imejiandaa mbele ya jaji Lucy Nyambura kuisikiliza kesi dhidi ya mbunge wa Matuga, Chirau Ali Mwakwere, Mwakwere hakufika kotini kama ilivyotarajiwa. Mwakwere alisema kuwa hakupewa mwito wa kumjulisha afike kotini tarehe 9 agosti mwaka 2012. Hata hivyo mmoja wa mawakili wanaowakilisha upande wa serikali , Lilian Obuo alisema kuwa mwakwere alikuwa anakwepa kuhudhuria vikao vya mahakama hasa ikizingatiwa kuwa hapo jana alizungumza na wanahabari kuhusiana na swala hili. Kulingana na afisaa wa uchunguzi, Salome Wachira, Mwakwere alisema kuwa angechukua ilani ya kumtaka kufika mahakamani kabla ya ilani hiyo kuwasilishwa kwake. Jaji Lucy Nyambura aliagiza kuwa Mwakwere atumiwe mwito rasmi, na kutakiwa kufika mahakamani tarehe 13 mwezi agosti, wakati ambapokesi yake itakaposikilizwa.