Kizaazaa kiliibuka mjini Kakamega hii leo baada ya familia moja kuchukua mwili usiokuwa wao na kuupeleka kanisani kwa ibada kabla ya mazishi. Wenyeji wa kijiji cha shironyanga walipigwa na butwaa walipogundua kuwa maiti waliokuwa wanaelekea kuizika ni ya mtu tofauti. Haya yote yakiendelea familia ya pili nao walikuwa wamejawa na hofu na hali ya kuchanganyikiwa wakidhani kuwa maiti ya jamaa yao ilikuwa imeibiwa. Mwanae marehemu agnes namusia, anasema palikuwa na vuta ni kuvute baina yake na dada zake kuhusu iwapo kweli walikuwa wamebeba maiti ya mama yao, na hapo ndipo wakauchukua mwili huo ambao ulikuwa wa mtu tofauti.iliwabidi kukatiza ibada na kurejesha maiti hiyo kwa jamaa zake.