Familia moja wilayani Nambale inaomboleza kifo cha mtoto wao wa kike aliyeteketea akiwa ndani ya nyumba. Babu yake msichana huyo anashukiwa kuhusika na mkasa huo huo wa moto baada ya mzozo wa ardhi kutokea baina yake na babake mtoto huyo . Mzee huyo ametiwa nguvuni huku akisubiri kufikishwa mahakamani .