Jamii ya Wamasaai hatimaye imefanya mkutano na Mkurugenzi wa Shirika la Wanyamapori nchini Julius Kipgetich. Kwa muda mrefu jamii hiyo imekuwa ikipanga kufanya mkutano na mkurugenzi huyo bila ya ufanisi wowote. Jamii hiyo inapania kutilia kikomo mzozo ambao umekuwa ukishuhudiwa baina yao na wanyama pori.miongoni mwa matakwa waliyoibua hii leo ni kupewa fidia kila mifugo yao pindi wanaposhambuliwa na wanyamapori kando na wao kutaka kunufaika kupitia mapato ya mbuga za wanyama.