Naibu Jaji Mkuu Nancy Barasa anafaa kutimuliwa kutoka ofisini, ndiyo mapendekezo ya Jopo lililochunguza kesi yake ya utovu wa nidhamu. Ripoti hiyo ya wanasheria hao 7 walioongozwa na Jaji mstaafu wa tanzania Augostino Ramadhan sasa itawasilishwa kwa Rais Mwai Kibaki ili ayatimize mapendekezo. Barasa alishtakiwa na mlinda lango Rebecca Kerubo mapema mwezi Januari kwa kumtishia maisha kwa kutumia bunduki na hata kumkejeli.