Afisa mmoja wa polisi ameuawa kwa kupigwa risasi katika mtaa wa umoja innercore usiku wa kuamkia jumamosi katika hali ya kutatanisha. Inadaiwa kuwa afisa huyo aliuawa na polisi wenzake na inasemekana amekuwa akiandamwa kwa mda kabla ya kuuwawa kwa kupigwa risasi na kufa papo hapo.