Shule ya Acacia Crest Academy eneo la kitengela imefungwa kufuatia ajali iliyosababisha vifo vya watoto watatu hapo jana. Waalimu, wanafunzi na wazazi wa shule hio walikutana kwa maombi kuomboleza familia, jamaa na marafiki wa wale walioaga dunia katika ajali hiyo, iliyosababishwa baada ya basi la shule hiyo kuvunja kanuni za barabani na kugongwa na matatu katika barabara kuu ya Mombasa, eneo la Sabaki.