Tume ya uchaguzi na mipaka iebc hii leo ilifika mbele ya tume ya utekelezaji wa katiba CIOC na kamati ya bunge kuhusu sheria kueleza ni kwanini walikatiza zabuni ya usajili wa wapiga kura kupitia mfumo wa elektroniki. Mwenyekiti wa tume hiyo isaack hassan alieleza kuwa kampuni zote walizofanyia uchunguzi hazikufaulu kupewa kandarasi hiyo. Kwa mujibu wa tume hiyo ni kwamba lengo lao kuu ni kuandaa uchaguzi wa huru na haki