Madakitari na wauguzi wa hospitali ya St.Mary’s katika mtaa wa Langata walifanya mgomo wakilalamikia kutatizwa katika utoaji huduma kufuatia mvutano baina ya mwanzilishi wa hospitali hiyo na kanisa katoliki. Aidha madakitari wawili wamekamatwa na polisi kwa madai ya kupuuza kesi inayoendelea mahakamani kuhusu umiliki wa hospitali hiyo. Isabella Kituri anatupasha zaidi.