Tume ya Uchaguzi na Mipaka IEBC imesitisha zoezi la utoaji wa zabuni ya vifaa vya usajili wa wapiga kura kupitia njia ya electroniki. Hatua hii imejiri baada ya wote waliokuwa wakiwania zabuni hiyo kushindwa kufaulu. Mchakato huu umekuwa wenye kuzingirwa na utata hasa baada ya madai kuibuka kwamba kampuni ya Sympony iliyokuwa ikifanyiwa uchunguzi ilikuwa imeorodheshwa na Bunge miongoni mwa kampuni ambazo hazifai kupewa kandarasi.