Mara nyingi katika maisha yetu kama wanadamu sisi hukutana na changamoto na vikwazo vingi ambavyo hutufanya tufe moyo na kukosa tamaa ya kuendelea na maisha. Lakini cha msingi kwetu ni kukabiliana na matatizo haya na kusukuma maisha mbele. Ndio uamuzi uliofanywa na jamaa mmoja aliyepofuka katika maisha yake ya utu uzima na kuhisi kuwa ndoto yake ilikuwa imekatizwa. Katika makala maalum, mwanahabari wetu Carol Nderi alizungumza na mwalimu mmoja kutoka Othaya, Paul Kiragu aliyepoteza uwezo wake wa kuona na kumbidi kubadilisha mkondo wake wa maisha.